

Afisa Mhamasishaji na Msemaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema uongozi wa timu hiyo utafanya maboresho ya mapungufu yote yaliyojitokeza kwenye kikosi cha timu hiyo
Nugaz alikuwepo uwanja wa Taifa jana kuishuhudia Yanga ikipepetana na KMC katika mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1
Akizungumza baada ya mchezo huo Nugaz alisema matokeo hayo ni sawa na kupoteza kwao lakini ni moja ya matokeo ya mpira wa miguu hivyo wanapaswa kuyasahau
"Vijana wamejitahidi kucheza vizuri ni makosa madogo yaliyojitokeza mwishoni yamepelekea tukose ushindi," alisema
"Naamini tutakuwa na timu imara zaidi baada ya dirisha dogo kwani tutakuwa na nafasi ya kuboresha mapungufu yaliyojitokeza kwenye timu yetu"
"Tunatarajia wachezaji watapewa mapumziko ya siku kadhaa kabla ya kurejea kambini ambapo tutatangaza ratiba ya michezo ya kirafiki ambayo tutacheza ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wetu wa January 04, 2020 dhidi ya Simba"
Kwa habari zaidi Download App ya soka kiganjani kutoka Play Store



0 Comments