Windows

Wachezaji Kili Stars waahidi kurudi na taji la Chalenji



Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' wameahidi kufanya kila linalowezekana kushinda taji la michuano ya Chalenji itakayofanyika nchini Uganda kuanzia mwishoni mwa wiki

Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari, mlinda lango Aishi Manula amesema baada ya kukosa ubingwa wa michuano hiyo kwa miaka mingi, kama wachezaji wanaona wana deni la kutwaa taji hilo

"Sisi kama wachezaji tumejiandaa kwenda kupambana kuipigania nchi yetu ili tuweze kupata matokeo chanya kwenye michuano hiyo"

"Mara ya mwisho kwa Tanzania Bara kushinda michuano hii ilikuwa mwaka 2010, ni muda mrefu kidogo umepita. Hivyo kwetu wachezaji tuna wajibu wa kuirudisha heshima ya nchi yetu kwa kushinda taji hilo," amesema

Nae kocha mkuu wa timu hiyo Juma Mgunda amesema wamefanya maandalizi ya kutosha kuweza kufanya vizuri kwenye michuano hiyo

"Tumejiandaa kwenda kushindana michuano ya Chalenji Kampala, hivyo tutakuwa tayari kukutana na timu yoyote kwenye michuano hiyo"

"Lengo letu ni kuhakikisha tunafanya vizuri katika michuano hiyo"

Kilimanjaro Stars itaondoka nchini kesho Alhamisi kuelekea Uganda kushiriki michuano hiyo

Kili Stars itaanza michuano hiyo kwa kuumana na ndugu zao Zanzibar Heroes katika mchezo utakaopigwa Jumapili Disemba 08

Katika hatua nyingine wachezaji Salum Abubakar, Shaban Iddi na Iddi Selemani 'Nado' wote wa Azam Fc wameondolewa kikosini baada ya kupata majeraha



Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.

Post a Comment

0 Comments