

Viwanja vya klabu ya Simba vilivyoko Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam vimekamilika ambapo uzinduzi unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii
Baada ya kazi kubwa ya kutandika kapeti katika kiwanja cha nyasi bandia kwa sasa mafundi wanaendelea na zoezi la usafi pamoja na kurekebisha maeneo ambayo hayako sawa
Aidha kazi hiyo inaenda sambamba na ujenzi wa uzio
Hakika ni jambo la kuvutia, Mwekezaji wa Simba Mohammed Dewji, Bodi ya Wakurugenzi na viongozi wanastahili pongezi nyingi kwa kufanikisha ndoto hii ya Wanamsimbazi kumiliki uwanja wao ingawa kwa sasa ni kwa ajili ya mazoezi tu
Lakini kukamilika kwa awamu ya kwanza kunatoa nafasi kwa kuanza kwa mchakato wa ujenzi wa awamu ya pili ambao utahusisha uwekaji wa majukwaa na Hostel za wachezaji
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.



0 Comments