

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wataanzia nyumbani raundi ya tatu ya michuano ya kombe la FA (ASFC)
Katika droo iliyofanyika mapema leo, Simba imepangwa kucheza na Arusha Fc kutoka mkoani Arusha
Mchezo baina ya timu hizo utapigwa uwanja wa Uhuru
Kwa misimu miwili mfululizo Simba haikuvuka raundi ya tatu lakini msimu huu uongozi umeweka wazi mapema kuwa wamepania kutwaa taji hilo
Hivyo michuano hiyo itapewa kipaumbele kama ilivyo michezo ya ligi
Michezo ya raundi ya tatu itapigwa kati ya Disemba 20-28 2019
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.



0 Comments