Windows

Simba, Yanga, Azam zapewa vibonde Kombe la FA

Simba-Yanga- Azam -zapewa -vibonde -Kombe la FA-Azam Sports Federation -mashindano ya Kombe -mwanasport-MwanaspotiSoka-MwanaspotiGazeti-
Vigogo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, Yanga na Azam wamepewa vibonde katika hatua ya tatu ya mashindano ya Kombe la FA maarufu Azam Sports Federation Cup (ASFC).


Katika Droo iliyopangwa leo imeshirikisha jumla ya timu 64: Timu 20 zinatoka ligi kuu, timu 24 kutoka ligi daraja la kwanza na timu 20 zilizofuzu kutoka madaraja ya chini.


Mabingwa watetezi Azam FC watakutana na African Lyon ya daraja la kwanza wakati Simba wakiwakaribisha Arusha FC ambayo hali yake ni tete kiuchumi huku Yanga watakuwa wenyeji wa Iringa United.


Kwa mujibu wa droo hiyo, mechi 32 za raundi ya tatu ambazo zitachezwa kati ya Desemba 22 hadi 28 mwaka huu ni kama ifuatavyo, Migombani itaikaribisha Mbeya City, Songwe, Polisi Tanzania itacheza dhidi ya Top Boys ya Ruvuma.


Mwadui FC watavaana na Mkamba Rangers kutoka Morogoro, Tukuyu Stars watacheza dhidi ya Singida United, Mbuni FC wao watacheza dhidi ya KMC, Alliance ya Mwanza watavaana na Transit Camp ya daraja la Kwanza, Ndanda SC watacheza dhidi ya Cosmo Politan.


Milambo FC ya Tabora ambayo ipo daraja la pili watacheza dhidi ya Ruvu Shooting, Mbao FC watacheza dhidi ya Stand United, Nyamongo wao watakuwa na kibarua kizito mbele ya ndugu zao Biashara United, Mawenzi Market dhidi ya Mtwivila.Mpwapwa United watacheza dhidi ya Kitayosa ya Tabora, Talinega FC ya Kigoma wataikaribisha Friends United, Ihefu watavaana na Kasulu Red Star, Toto Africans ya Mwanza dhidi ya Gipco, Mighty Elephant wao watachuana na Mashujaa FC, Jeshi Warriors watacheza dhidi ya Dodoma FC.


Majimaji FC watachauana na Pamba SC, Panama FC dhidi ya Area C, Gwambina FC watakuwa na kibarua mbele ya Mbeya Kwanza, Pan African watacheza dhidi ya Geita Gold, Njombe Mji wakiwa nyumbani Ruvuma wataikaribisha Sahare All Stars.


Lipuli FC watacheza dhidi ya Dar City, Kagera Sugar watakuwa na kibarua dhidi ya Rufiji United,Tanzania Prisons watakuwa Sokoine kucheza dhidi ya Mlale FC, Mtibwa Sugar wao ni dhidi ya Rhino Rangers.


Tanga nako kutakuwa na dabi kati ya Coastal Union dhidi ya African Sports, Namungo FC watachuana na Green Warriors wababe wa Simba msimu uliopita hao, JKT Tanzania watacheza dhidi ya Boma FC ya Mbeya.





Post a Comment

0 Comments