

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes' Hemed Morocco ametaja majina ya wachezaji 25 ambao wanaelekea nchini Uganda kushiriki michuano ya CECAFA Seniro Chalenji
Awali Morocco aliita nyota 40 kabla ya kufanya mchujo na kuwapata nyota 25
Nyota wanne wa Yanga Alli Alli, Abdulaziz Makame, Mohammed Issa na Feisal Salum wote wamejumuishwa katika kikosi hicho cha nyota 25
Zanzibar Heroes itaanza michuano hiyo kwa kuchuana na ndugu zao Tanzania Bara katika mchezo ambao utapigwa Jumapili Disemba 08
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.



0 Comments