Windows

Ninja ashangaa kiwango cha Yanga mechi dhidi ya KMC



Beki wa LA Galaxy ya Marekani, Abdallah Shaibu 'Ninja' jana alikuwepo jukwaani akishuhudia Yanga ikilazimishwa sare 1-1 na KMC

Ameeleza kushangazwa jinsi timu yake hiyo ya zamani ilivyocheza soka la kupooza.

Ninja aliyeichezea Yanga kabla ya kujiunga na LA Galaxy mwanzoni mwa msimu amerejea nchini katika mapumziko wakati huu Ligi ya Marekani imesimama kupisha majira ya baridi.



Akizungumzia mechi hiyo, Ninja alisema katika mchezo huo ameona walikuwa wanacheza kwa kupooza kama vile wachezaji wamechoka, kitu ambacho si kizuri kwa Yanga inayohitaji ubingwa.

"Si Yanga wala KMC, walicheza kwa kupooza sana, imeonekana kama wachezaji wamechoka pengine ratiba ya ligi inawabana, ila wanahitaji kujitofautisha na timu nyingine ili kuchukua ubingwa,"

"Wachezaji wazawa wajaribu kuwapa nafasi, kwani wanakuwa wanajua ligi ilivyo kuliko wageni ambao nimeona wanakwama kidogo," alisema Ninja.

Jambo lingine ambalo alikuwa makini sana kulifafanua kwamba hataki kuingilia majukumu ya benchi la ufundi ila alishauri wachezaji wangecheza kwenye namba zao akimtolea mfano Jafary Mohamed

Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.

Post a Comment

0 Comments