Windows

Nimefuata ubingwa Simba - Vanderbroeck



Kocha Mkuu wa Simba Sven Vanderbroeck amesema kilichomleta nchini ni kazi moja tu, kuhakikisha anaipa Simba mafanikio

Vanderbroeck amesema amekuja kukamilisha malengo makubwa msimu huu ambayo ni kutetea ubingwa wa ligi kuu

Ubingwa utaihakikishia Simba nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao

Kocha huyo raia wa Ubelgiji amesema kuwa anafahamu Simba ni klabu kubwa, mashabiki wake wanataka kuona timu yao ikifanya mambo makubwa pia

"Nimekuja Simba ili kushinda ubingwa, lengo langu tucheze Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao, najua Simba ni timu kubwa na mashabiki wake wanataka mambo makubwa," amesema



Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.

Post a Comment

0 Comments