

Wingi wa Kamati klabu ya Yanga umeanza kuibua maswali miongoni mwa mashabiki wa wadau wa klabu hiyo
Jana Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla alitangaza kuundwa upya kwa Kamati ya Mashindano ambayo inaundwa na Wajumbe 13
Tangu Dk Msolla aingie madarakani Mei 5 mwaka huu, ameunda Kamati tano na kufanya Yanga iwe na Kamati tisa!
Kamati nyingine ni Kamati ya Usajili, Kamati ya Sheria na Nidhamu, Kamati ya Matawi ya Wanachama, Kamati ya Kudumu ya Hamasa, Kamati ya Ufundi na Kamati ya Ujenzi
Pamoja na kuwa kila Kamati ina umuhimu wake, wengi wameonyesha hofu juu ya gharama ambazo Kamati hizi pengine zinatumia katika utendaji wake
Kutokana na hali ya kiuchumi ya Yanga, wapo wenye wasiwasi wingi wa kamati unaipelekea Yanga kujiingiza katika gharama zisizo za lazima labda kama wajumbe wa Kamati hizo wanafanya kazi kwa kujitolea
Lakini pia baadhi ya Kamati bado hazijaonyesha ufanisi huku nyingine zikiundwa na kuvunjwa baada ya muda
Hata ukiangalia Wajumbe wa Kamati hizi mara nyingi ni walewale wamekuwa wakihamishwa tu kutoka Kamati moja kwenda nyingine
Dk Msolla ashauriwe kuwa ili kuongeza ufanisi Yanga sio lazima kuwa na utitiri wa Kamati
Anaweza kuwa na Kamati chache lakini zenye wachapakazi ambao watamrahisishia kazi
Dk Msolla akumbuke kuna ahadi nyingi aliwapa Wanachama wa Yanga na hivyo kumchagua kwa kishindo
Sasa ni zaidi ya miezi sita, wengi bado wanasubiri utekelezaji wa zile ahadi muhimu



0 Comments