Windows

Majembe sita kutua, sita kuachwa Yanga




Kuelekea usajili wa dirisha dogo klabu ya Yanga inatarajiwa kuboresha kikosi chake katika jitihada za kujiimarisha kwenye mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu walioupoteza kwa watani zao Simba kwa misimu miwili

Mabingwa hao wa kihistoria huenda wakaachana na nyota sita ambao wameshindwa kuonyesha makali

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema tayari wameshapokea ripoti ya Mwalimu kuhusu maboresho ambayo wanapaswa kuyafanya

"Tunayo orodha ya wachezaji ambao tunaweza kuachana nao dirisha dogo, tutazungumza nao kulingana na mikataba yao ili tuweze kuachana nao vizuri," amesema

"Majina yao tutayatangaza baadae baada ya kuwa tumemalizana nao"

Kuhusu nafasi ambazo watazifanyia maboresho, Mwakalebela amesema katika usajili ambao watafanya ni pamoja na kuboresha eneo la ushambuliaji na safu ya ulinzicut

Amesema usajili utakaofanyika unaweza kujumuisha wachezaji watatu wa kigeni na watatu wazawa

Miongoni mwa nyota wa kigeni wanaohusishwa na Yanga dirisha dogo ni Haruna Niyonzima (AS Kigali-Rwanda), Erick Rutanga(Rayon-Rwanda), Michael Sarpong(Rayon-Rwanda) na Yacouba Songne (rasta wa Asante Kotoko)

Nyota wazawa ni pamoja na Bakari Mwamnyeto (beki-Coastal Union), Ismail Aziz (winga-Prisons) na Cleophas Mkandala (kiungo-Prisons)

Post a Comment

0 Comments