

Kesho Jumatano Kocha Etienne Ndayiragije atatangaza majina ya wachezaji wanaounda kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' ambacho kitashiriki michuano ya CECAFA Challenge itakayoanza Disemba 07 2019 nchini Uganda
Mlinda lango namba moja wa Simba Aishi Manula hakujumuishwa katika kikosi cha Stars tangu aumie kwenye michuano ya Afcon 2019 iliyofanyika mwezi Julai mwaka huu nchini Misri
Wengi wamekuwa wakijiuliza kwa nini Manula amekuwa hajumuishwa timu ya Taifa siku za karibuni
Akihojiwa na eFM mapema leo, Ndayiragije ametaja sababu ya Manula kutojumuishwa kikosini kuwa mlinda lango huyo aliomba apewe mapumziko kutokana na majeraha yaliyokuwa yakimsumbua
"Nilimuita Aishi Manula kwenye mechi ya Kenya na baada ya siku mbili akanieleza hayupo sawa kiafya anahitaji muda wa kupumzika," amesema Ndayiragije
"Aishi alitoka vizuri,Tupo naye vizuri na nimemuangalia yupo vizuri kwa sasa bado ni mchezaji bora"
Je atamjumuisha kwenye kikosi kitakachoelekea Uganda wiki ijayo? tusubiri..



0 Comments