

Gazeti moja la michezo leo imeripoti kuwa mshambuliaji wa Yanga Sadney Urikhob ametoweka katika klabu hiyo
Uongozi wa Yanga umekanusha taarifa hiyo na kuthibitisha kuwa mchezaji huyo leo ameshiriki mazoezi ya asubuhi ambayo yamefanyika uwanja wa Uhuru
"Sadney ameshiriki mazoezi ya Yanga yaliyofanyika uwanja wa Uhuru leo, yuko ‘fit’ na hajawahi kukosa mazoezi ya timu tangu Novemba 5, 2019," imesema taarifa ya Yanga



0 Comments