

Kaimu Mwenyekiti wa klabu ya Simba Mwina Kaduguda amesema Mwekezaji wa klabu hiyo Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' ameshaingiza kiasi cha Tsh Bilioni 20 za uwekezaji kwenye akaunti ya klabu ya Simba
Kukamilika kwa hatua hiyo ni ishara kwamba mchakato umekamilika ambapo hatua itakayofuata ni uuzwaji wa hisa asilimia 51 kwa Wanachama
Mo anamiliki hisa asilimia 49 ambazo thamani yake ni Tsh Bilioni 20
Mchakato wa fedha hizo kuingizwa kwenye akaunti ya Simba ulichelewa kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya masuala ya kisheria



0 Comments