

Bodi ya Wakurugenzi ya Simba inatarajiwa kukutana Novemba 28 kujadili masuala mbalimbali likiwemo la kocha mkuu wa timu hiyo Patrick Aussems
Mmoja wa Wajumbe wa Bodi hiyo amesema Aussems anakabiliwa na mashitaka mawili, mosi safari yake ya ghafla aliyofanya mapema wiki hii na pia kitendo cha kutohudhuria kikao baina yake na Mtendaji wa Simba Senzo Mazingisa pamoja na Kaimu Mwenyekiti Mwina Kaduguda
Inaelezwa baada ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambao Simba ilishinda kwa mabao 3-0, Aussems alitaarifiwa rasmi juu ya kutakiwa kuhudhuria kikao hicho
Aidha taarifa zaidi zimebainisha kuwa kocha huyo raia wa Ubelgiji amesimamiwa kwa muda mpaka hapo kitakapofanyika kikao hicho



0 Comments