

Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere na Emmanuel Okwi ambaye aliitumikia Simba msimu uliopita wametajwa miongoni mwa wanaowania tuzo ya Mwanasoka Bora kutoka ndani ya Afrika ngazi ya vilabu
Kagere alikuwa mmoja wa wafungaji bora wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu uliopita akiisaidia Simba kutinga robo fainali ya michuano hiyo
Okwi ambaye kwa sasa anasakata kabumbu nchini Misri, uteuzi wake umetokana na mafanikio aliyopata wakati yuko na Simba msimu uliopita
Wachezaji 20 kutoka vilabu mbalimbali barani Afrika wameteuliwa kuwania tuzo hiyo



0 Comments