Windows

Baada ya kipigo Massau Bwire agoma kupokea zawadi ya Manara



Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara aliazimia kumpatia simu mpya ya 'iPhone' msemaji mwenzake wa klabu ya Ruvu Shooting Massau Bwire

Kabla ya mchezo wa ligi kuu kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Simba hapo jana, Bwire alisikika akitoa tambo nyingi kuwa timu yake itaibuka na ushindi

Hata hivyo baada ya kipigo cha mabao 3-0 jana, Massau alibadili kauli na kusema 'meli ilizidiwa na mzigo' hivyo ikazama

Manara aliahidi kumpatia zawadi hiyo ya simu ili aachane na utaratibu wa kutembea na idadi kubwa ya simu

"Bwire chagua simu ipi unataka, kuna iPhone 10 na 11 halafu niambie nikaiache wapi shuleni au mabatini," alisema Manara

Hata hivyo Massau amegoma kupokea zawadi hiyo

"Simu ni kitu gani, mawasiliano tu brother, simu zangu ni ndogo kiumbo lakini ni kubwa kiuwezo"

Post a Comment

0 Comments