Windows

Mkwasa ana kazi kuimarisha safu ya ulinzi



Wakati wa Zahera Yanga ilikuwa ikionekana kukosa mipango ya kutengeneza mabao hivyo kutegemea zaidi mipira ya kona, adhabu na penati kufunga mabao yake

Kocha Charles Mkwasa ambaye anakaimu nafasi ya kocha Mkuu, kwa kiasi kikubwa ameonyesha kuelekea kutibu 'gonjwa' hilo kwani kwenye michezo ya hivi karibuni Yanga imekuwa ikifunga mabao mengi

Timu inaonekana kuwa na mipango, inatengeneza nafasi nyingi, chache zinatumiwa ingawa bado sio kwa kiwango cha kuridhisha lakini si haba

Hata hivyo bado kuna changamoto kwenye safu ya ulinzi au mfumo wa kujilinda kwa ujumla pale timu inaposhambuliwa

Kwani katika michezo miwili iliyopita pamoja na kufunga mabao sita, Yanga imeruhusu mabao matatu

Mkwasa amekiri uwepo wa changamoto hiyo ambapo katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania alisema mlinda lango Farouk Shikhalo hakuwa na mawasiliano mazuri na walinzi wake hivyo kupelekea kuruhusu kufungwa mabao mepesi

Mkwasa ana kazi ya kuhakikisha anamaliza makosa ya safu yake ya ulinzi ili kuweza kujihakikishia kushinda mechi nyingi

Msimu huu Yanga ina uwiano usioridhisha wa mabao, imefunga mabao tisa na kuruhusu mabao sita!

Post a Comment

0 Comments