

Kaimu Mwenyekiti wa klabu ya Simba Mwina Kaduguda amesema atamshawishi Mwekezaji wa klabu hiyo Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' kujenga kituo cha michezo 'Academy' eneo la Bunju ambalo Simba tayari inamiliki viwanja viwili
Kaduguda amesema umiliki wa Academy utaisaidia Simba kujikita katika ufundi wa mpira
Lakini pia timu itanufaika katika kulea wachezaji ambao baadae wataitumikia na wengine kuuzwa na kuipatia timu mapato
"Ili tuwekeze katika ufundi wa mpira, tunatakiwa tuwe na Youth Program, Mimi nitamshawishi Mwekezaji wa Simba tujenge kitu kinachoitwa Simba Sports Club Sports Complex," amesema
"Humo kwenye Sports Complex kutakuwa na kituo cha michezo ambacho ndani yake kutakuwa na shule za Chekechea, Msingi na Sekondari pamoja Chuo vyote vikimilikiwa na klabu ya Simba"
Huu ndio utaratibu ambao unatumiwa na vilabu vikubwa duniani, kama Simba itafanikiwa kujenga kituo hicho itakuwa klabu ya kwanza kufanya hivyo Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki na kati



0 Comments