Baada ya kupoteza matumaini ya kumnasa mshambuliaji Ditram Nchimbi anayecheza kwa mkopo Polisi Tanzania akitoka klabu ya Azam Fc, Yanga imeanza kuwafuatilia mshambuliaji wa Lipuli Fc Daruweshi Saliboko na Tariq Seif Kiakala anayecheza nchini Misri
Mapema wiki hii uongozi wa Azam Fc uliweka wazi kuwa Nchimbi bado ana mkataba wa miezi minane na timu hiyo, timu zinazotaka huduma yake zinapaswa kuwasiliana na matajiri hao wa Chamazi
Yanga inatarajiwa kuongeza nguvu katika safu yake ya ushambuliaji ambapo taarifa zinabainisha kuwa wamepanga kuongeza washambuliaji wawili, mmoja mzawa na mwingine wa kigeni
Saliboko anaweza kuwa chaguo sahihi kwani ni mmoja wa wachezaji wanaofanya vizuri ligi kuu ya Vodacom msimu huu
Nyota huyo ameifungia Lipuli Fc mabao sita katika mechi 10 alizocheza
Tariq yeye aliwahi kuzitumikia Stand United na Biashara United kabla ya kutimikia Misri ambako amejiunga na timu ya daraja la pili, Dekernes Fc
Meneja wa mchezaji huyo Abdulrahman Fumbwe amesema Yanga wamemuulizia mteja wake na wako tayari kumchukua hata kwa mkopo
Tariq ameonyesha kiwango kizuri katika timu yake nchini Misri
Katika maandalizi ya msimu mpya, Tariq alicheza michezo 7, alifunga magoli 5 na kutoa pasi 3 za magoli
Pia kuna uwezekano mkubwa Yanga ikamrejesha aliyekuwa winga wake mshambuliaji Yusuf Mhilu ambaye anaitumia klabu ya Kagera Sugar aliyojiunga nayo mwanzoni wa msimu akitokea Ndanda Fc ambako Yanga ilimpeleka kwa mkopo
Mhilu amekuwa na msimu mzuri mpaka sasa akiwa ameifungia Kagera Sugar mabao matano, ndiye kinara wa mabao katika kikosi cha Kagera Sugar kinachonolewa na Meckie Mexime
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments