Mabeki Kelvin Yondani na Lamine Moro leo wanatarajiwa kuongoza ngome ya ulinzi ya Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Alliance Fc ambao utapigwa uwanja wa CCM Kirumba
Mara ya mwisho mabeki hao kucheza pamoja ulikuwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Zesco United nchini Zambia, mchezo ambao Lamine alitolewa nje kwa kadi nyekundu
Kadi nyekundu hiyo ilimfanya asicheze mchezo wa kwanza wa mtoano kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc ambao ulipigwa jijini Mwanza
Katika mchezo huo nae Yondani akapata kadi nyekundu hivyo kukosa mchezo wa marudiano nchini Misri, mchezo ambao Lamine alirejea kikosini
Leo kocha Charles Mkwasa huenda akawarejesha wawili hao kati na pengine atampeleka pembeni Ally Mtoni
Katika mchezo uliopita dhidi ya JKT Tanzania, Mtoni na Lamine walicheza pamoja kati lakini walionekana kukosa maelewano pamoja na mlinda lango Farouk Shikhalo
Kurejea kwa Yondani kutaongeza umakini kwenye safu ya ulinzi
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments