Tetesi zimekuwa nyingi kuhusu benchi la ufundi la Simba, huku Bodi ya Wakurugenzi ikitarajiwa kukutana leo kufanya maamuzi
Jana kocha Mkuu Patrick Aussems alifikishwa mbele ya Kamati ya Nidhamu kujibu tuhuma mbalimbali zinazomkabili
Inaelezwa baada ya kikao hicho ambacho kilikuwa na mvutano wa hapa na pale, Kamati ya nidhamu leo itawasilisha ripoti yake kwa Bodi ya Wakurugenzi kwa ajili ya maamuzi
Kikao kinatarajiwa kufanyika saa 11 jioni
Wakati hayo yakiendelea, tetesi za mabadiliko ya benchi la ufundi zimeendelea kushika kasi ambapo kocha wa Polisi Tanzania Selemani Matola anatajwa kuwa njiani kurejea Msimbazi katika nafasi ya kocha Msaidizi
Taarifa zinabainisha kuwa Simba huenda itavunja benchi lake la ufundi
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store
0 Comments