MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Eliuter Mpepo anayekipiga katika timu ya Buildcon ya Zambia amefunguka kuwa Yanga wanayo nafasi ya kuibuka na ushindi dhidi ya Zesco United ikiwa imefanya maandalizi makubwa kutokana ukubwa wapinzani wao.
Timu hizo zinatarajiwa kucheza mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika, kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa uliopo Ndola, Zambia, baada ya sare ya bao 1-1 ya katika mchezo wa kwanza.
Mpepo amesema kuwa Yanga wanaweza kupata matokeo ya ushindi ikiwa wamejiandaa vizuri kutokana na wapinzani wao kutokuwa na rekodi ya kufungwa kwenye uwanja wao nyumbani.
“Unajua mchezo wa soka upo tofauti na unavyoongelewa kwa sababu ukiangalia Zesco hawajawahi kupoteza mchezo wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani, jamaa wanakuwa na wakali sana jambo ambalo Yanga wanapaswa kulielewa.
“Lakini nafahamu ukubwa wa Yanga na kama watakuwa wamejiandaa basi wanaweza kupata matokeo kitu ambacho kinawezekana kwa kuwa soka ni mchezo wa makosa na Yanga hakuna asiyejua kwamba ni wazuri zaidi wanapokuwa ugenini ingawa ina wachezaji wengi ambao bado ni wapya,” alisema Mpepo.
INAITWA JEURI YA PESA..! WEMA SEPETU Apewa Zawadi ya GARI na Aunt Ezekiel
The post Straika Zambia: Zesco Wanafungika, Yanga Wakaze appeared first on Global Publishers.
0 Comments