VIRGIL van Dijk ni mmoja wa mabeki bora wa kati katika mchezo wa soka kwa sasa, lakini kumekuwa na maswali mengi kuhusu uamuzi wa kutumia jina lake la kwanza kwenye jezi badala ya lile la pili ambayo ni maarufu zaidi.
Habari ni kuwa kuna sababu kubwa na ya muhimu ambayo imesababisha beki huyo anayeshikilia Tuzo ya Beki Bora Ulaya kuchukua uamuzi huo na siyo kwamba imetokea kwa bahati mbaya.
Van Dijk anatumia jina la Virgil kwenye jezi zake kwa kuwa hana uhusiano mzuri na baba yake, kwani alitalikiana na mama yake wakati yeye akiwa mdogo na hakuwa na muda na familia yake hiyo.
Hayo yamese-mwa na mjomba wa Virgil anayefa-hamika kwa jina la Steven Fo Sieeuw.
“Baba yake alimuacha mama yake huku akiwa na watoto watatu, maisha yalikuwa magumu kwa Virgil, baba hakuwepo kutoa msaada badala yake mama ndiyo alikuwa kila kitu na hiyo ndiyo sababu,” alisema mjomba huyo.
The post Siri ya Van Dijk kutumia jina la Virgil hii hapa… appeared first on Global Publishers.
0 Comments