Windows

Simba, Yanga wakutana uzunguni

KATIKA hali ya kushangaza, juzi Jumamosi wachezaji wa timu ya Yanga na Simba walikutana sehemu moja ya mazoezi jambo ambalo lilizua tafrani kwa mashabiki wa timu hizo.

 

Simba ambayo inajiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar Alhamisi ya wiki hii, ilikutana na Yanga kwenye Uwanja wa Gymkhana jijini Dar.

 

Katika uwanja huo ambao upo maeneo ya ‘uzunguni’, juzi Yanga ilikwenda mapema uwanjani hapo kwa ajili ya maandalizi yao ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco United.

 

Akizingumza na Championi Jumatatu, Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh alisema kuwa hiyo si mara ya kwanza kwao kukutana kwenye viwanja vya mazoezi kwa kuwa hakuna anayemiliki wa kwake zaidi ya kufanya kazi ya kukodi.

 

“Hakukuwa na tatizo sisi kukutana na Simba pale Gymkhana kwanza ieleweke hakuna kati yetu anayemiliki, wote tunafanya kazi ya kukodi ili timu iweze kufanya mazoezi ya kila siku.

 

“Lakini kilichotokea ni kwamba Simba kwa juzi hawakuwa na programu ya mazoezi ya ule uwanja na wao walikuja kwa ajili ya kwenda Gym ambayo ipo ndani ya Gymkhana ila siyo mara ya kwanza sisi na wao kukutana kwenye sehemu za mazoezi, tushakutana Boko Veterani na hata Uhuru, ingekuwa kule Bunju kwenye uwanja wao ndiyo ingeleta shida,” alisema Saleh.

Ibrahim Mussa, Dar es Salaam

The post Simba, Yanga wakutana uzunguni appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments