Timu za Ruvu Shooting, Mwadui Fc na Mtibwa Sugar zimetakiwa kutafuta viwanja vingine kwa ajili ya michezo yao ya nyumbani ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya viwanja vyao kufungiwa kwa kutokidhi vigezo
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema viwanja vya Manungu (Mtibwa Sugar), Uwanja wa Mwadui na kile cha Mabatini kinachotumiwa na Ruvu Shooting havitaruhusiwa kutumika mpaka vitakapofanyiwa ukarabati
Ruvu shooting itautumia uwanja wa Meja Samoyo uliopo Mbweni Jijini Dar es salaam
Mwadui Fc yenyewe itautumia uwanja wa CCM Kambarage wakati Mtibwa Sugar inahamia uwanja wa Jamhuri
0 Comments