Wakati uongozi wa Yanga ukihaha kupata vibali vya wachezaji wake wa Kimataifa Farouk Shikalo na Mustapha Suleyman, mshambuliaji David Molinga huenda akasubiri zaidi mpaka raundi ya pili kuweza kuitumika Yanga kwenye michuano ya ligi ya mabingwa
Usajili wa Molinga ulichelewa hivyo kukosa sifa ya kucheza michezo ya raundi ya awali kulingana na kanuni za CAF
Wachezaji wote watatu hawakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilicholazimishwa sare ya bao 1-1 na Township Rollers Jumamosi iliyopita
Molinga aliandikishwa kwenye mfumo wa usajili CAF nje ya muda wa kawaida wa usajili ambapo Yanga ililazimika kulipa faini ya dola 500
Hata hivyo yapo matumaini ya kupatikana vibali vya Shikalo na Mustapha ambao waliandikishiwa mapema lakini vibali vyao vimecheleweshwa na masuala ya kiofisi
Licha ya kuchelewa kuanza kuitumikia Yanga kwenye michuano ya CAF, Molinga hana kikwazo cha kuitumikia Yanga kwenye ligi
0 Comments