Uongozi wa Yanga ulifanya uamuzi sahihi wa kuweka kambi mkoani Kilimanjaro kujiandaa na mchezo dhidi ya Township Rollers
Kwa sasa baridi ni kali sana Moshi, hali ya hewa ambayo inaendana na hali ya hewa ya Botswana
Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema kambi hiyo itawasaidia wachezaji kutopata usumbufu watakapokwenda Botswana
Aidha, Saleh amesema kikosi cha timu hiyo kitaondoka Jumanne ijayo August 20 kuelekea Botswana
Aidha, aliongeza kuwa jana wachezaji wao walishindwa kufanya mazoezi ya asubuhi kutokana na baridi kali
"Hali ya hewa huku ni baridi kali, jana asubuhi wachezaji walishindwa kufanya mazoezi kutokana na hali hiyo lakini walifanya mazoezi jioni. Itatusaidia kuzoea mazingira haya ambayo tutakutana nayo Botswana" amesema
"Tunatarajia kuondoka Agosti 20, safari yetu itaanzia KIA, kikubwa tunakwenda kupambana"
Yanga imeweka kambi mkoani Kilimanjaro ili kuzoea hali ya baridi inayoelezwa kufanana na ile ya Botswana kwa sasa
0 Comments