TIMU ya Ruvu Shooting imetamba kuwa, inajipanga vyema kuhakikisha inafungua vema pazi la Ligi Kuu Tanzania Bara, kwa kupata ushindi katika mchezo wa kwanza dhidi ya Yanga.
Shooting inatarajia kushuka dimbani Agosti 28, mwaka huu kuikabili Yanga, katika mchezo wao wa kwanza wa ligi hiyo, utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, alisema kikosi chao kipo kambini kikiendelea na mazoezi pamoja na kucheza michezo ya kirafiki, kwa ajili ya kuhakikisha kinanoa makali yao vema kuelekea mchezo huo.
Alisema hadi sasa wamecheza michezo mitano ya kirafiki, ikiwemo dhidi ya Azam FC na Kombine ya Jeshi, huku wakiwa na mpango wa kucheza michezo mingine mingine miwili dhidi ya timu za Namungo na Polisi Tanzania.
“Wachezaji wamekaa kambini kipindi kirefu wakifanya mazoezi ili kujiweka katika hali ya ushindani, pia klabu imefanya usajili wa wachezaji 28 na 11 wakiwa ni vijana wapya ambao wanauwezo mkubwa.
“Tumejipanga vizuri kuhakikisha tunaanza msimu vizuri, tunajua ukubwa na ubora wa Yanga, lakini safari hii tunakuja kivingine kwa kuwa tuna kocha mzuri na mzoefu, hivyo hawawezi kutusumbua,nina hakika tutafungua vema msimu huu kwa ushindi,”alisema Bwire.
NA HELLEN GERALD (TUDARCo)

0 Comments