Windows

Aussems atamba, Simba imepata tiba ya michezo ya ugenini



Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema ana matumaini makubwa kuwa timu yake msimu huu itakuwa bora kwenye michuano ya ligi ya mabingwa kuliko msimu uliopita

Aussems amesema wamefanya kazi kubwa ya kujiimarisha kimfumo hasa wanapocheza ugenini

"Msimu uliopita hatukuwa na matokeo mazuri kwenye michezo ya ugenini. Ukiondoa mchezo dhidi ya Mbabane Swallows, tulipoteza michezo yote tuliyocheza ugenini," amesema

"Lakini msimu huu tumefanya maboresho, kwa kiasi kikubwa tumefanikiwa kwani kwenye mchezo wetu wa kwanza hatukuruhusu bao"

"Bado tunajiimarisha zaidi lakini nadhani msimu huu tutakuwa imara sana katika michezo ya ugenini kwenye ligi ya mabingwa"

Simba imeanza vyema kampeni ya ligi ya mabingwa msimu huu kwa kulazimisha suluhu ya bila kufungana dhidi ya UD Songo katika mchezo uliopigwa Msumbiji

Mabingwa hao wa Tanzania Bara watarudiana na UD Songo uwanja wa Taifa, August 25 2019

Kwa sasa kikosi cha Aussems kinaendelea na maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa keshokutwa dimba la Mkapa

Post a Comment

0 Comments