Kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc, Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema atafanya mabadiliko ya kikosi alichotumia katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya UD Songo
Akizungumza jana baada ya mazoezi ya kikosi cha Simba yaliyofanyika viwanja vya Gymkhana, Aussems amesema katika mchezo huo atafanya mabadiliko kidogo
Kwenye mchezo dhidi ya UD Songo uliopigwa Jumamosi iliyopita, Aussems aliwatumia Beno Kakolanya, Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Paschal Wawa, Jonas Mkude, Clatous, Sharaff Shibout, John Bocco, Meddie Kagere na FRancis Kahata
Hassani Dilunga, Mzamiru Yassini na Deo Kanda waliingia baadae kuchukua nafasi za Kahata, Chama na Mkude
Walinzi Mohammed Hussein, Gerson Fraga na Tairone Santos hawakupata nafasi ya kucheza kwenye mchezo huo
Kenedy Juma, Haruna Shamte na Miraji Athumani hawakusafiri kabisa na timu wakati Wilker Da Silva, Ibrahim Ajib na Aishi Manula waliondolewa kikosini kwa kuwa walikuwa majeruhi
Manula, Ajib na Da Silva watakosa mchezo huo utakaopigwa Jumamosi saa 1 jioni hivyo walinzi Kennedy Juma, Haruna Shamte na winga Miraji Athumani huenda wakapata nafasi kwenye kikosi cha kwanza
Aussems amesema mchezo dhidi ya Azam Fc ni muhimu kwa timu yake kwani ushindi utawahakikishia taji la kwanza msimu huu
Amesema baada ya mchezo huo watahamishia nguvu zao kuelekea mchezo dhidi ya UD Songo ambao utapigwa uwanja wa Taifa August 25
0 Comments