Windows

Waamuzi Ligi Kuu Bara kilio




KAMATI ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imepunguza idadi ya waamuzi wataocheza Ligi Kuu Tanzania Bara, msimu wa 2019/2020 kutoka 78 hadi 68.

Ligu Kuu Bara inatarajia kuanza Agosti 23, mwaka huu ikihusisha timu 20.

Akizungumza na MTANZANIA, Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Salum Chama, alitaja sababu iliyowafanya kupunguza waamuzi hao ni kuongeza ufanisi.

Chama alitaja kigezo kilichotumika kuwaondoa waamuzi 10 kuwa ni kufanya vibaya katika michezo iliyopewa nafasi hiyo.

“Tumeamua kupunguza waamuzi kwa sababu nyingi, kubwa ikiwa kutaka kufanya kuongeza ufanisi. Msimu uliopita tulikuwa na waamuzi wa kati 28, na wa pembeni walikuwa 50.

“Baada ya mchakato huo wa kuunda timu mpya ya waamuzi, msimu ujao wa kati watakuwa 24, pembeni 44, tuliangalia zaidi utendaji wao kazi wa msimu uliopita, wale waliofanya vibaya ndio tumewaondoa ila hatuwezi kuwataja kwa majina kwa sasa,”alisema.

Chama aliendelea kufungua kwa kusema wameweka sheria kali ya kuwabana waamuzi kwa msimu ujao, ambapo watakuwa wanafuatilia kuanzia mechi ya kwanza na atakayebainika kwenda kinyume watamuondoa haraka.

“Hatutamvumilia mwamuzi atakayekwenda kinyume na kanuni, yapo makosa ya kibinadamu yanaweza kutokea, lakini tukibaini mwamuzi amepindisha sheria huku akifahamu, tutamfuta moja kwa moja.

“Mfano kuna mambo ya kukataa goli ambalo ni halali, au kutoa kadi kwa mchezaji isiyostahili, kwa kweli mwamuzi kama huyo mara moja tutaanza naye, lengo ni kuboresha sekta hii,” alisema

Kamati hiyo imekuja na maamuzi hayo ikiwa tayari, Shirikisho la Soka Afrika, limefanya mabadiliko ya kanuni mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments