KOCHA Mkuu wa Azam FC, Etienne Ndayiragije, amesema akiwafunga Burundi katika mchezo wao wa Septemba 4, mwaka huu ugenini, kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2012, furaha yake haitaelezeka.
Ndayiragije ni mzaliwa wa Burundi hivyo katika mchezo huo, timu ya taifa lake hilo, itakuwa inavaana na timu anayoifanyia kazi.
Akizungumza na BINGWA jana, Ndayiragije alisema japo anatokea Burundi, lakini furaha yake ni kuona ameifunga nchi yake hiyo.
“Ninahitaji kuwafunga Burundi kwa hali yoyote, nikifanikisha hilo, nadhani furaha yangu haitaelezeka,” alisema.
Alisema yeye kuwa na timu ya Taifa ya Tanzania, inamaanisha kuwa ni mtanzania, hivyo kwenye hali ya kawaida, hawezi kuiacha timu yake anayoinoa ipoteze kirahisi.
Alisema anatamani kuiona Taifa Stars ikifika mbali na hata kufuzu fainali hizo za Kombe la Dunia ikiwa chini yake akiamini hilo linawezekana.
0 Comments