Windows

Kipaumbele ni kuhuisha teknolojia ya viwanda nchi za SADC - Rais Magufuli


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli amefungua maonesho ya wiki ya viwanda kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Africa (SADC).

Akizungumza katika hafla hiyo ya Wiki ya Viwanda ya SADC, Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema kuwa ili kufikia uchumi wa kati viwanda ni kichochea muhimu katika sekta nyingi kwani uwepo wa viwanda utasababisha uhakika wa uzalishaji na uchakataji wa bidhaa na kufanyabiashara kwa nchi wananchama.

Rais Magufuli amezitaka nchi wanachama wa SADC kuweka kipaumbele kwenye kuhuisha teknolojia katika viwanda vilivyoko ndani ya jumuiya ya Maendelea kusini mwa afrika (SADC) pamoja na kushughulikia kwa haraka zaidi vikwazo vinavyochelewesha ukuaji wa viwanda.

“Viwanda ni Sekta muhimu katika kukuza uchumi wa nchi yeyote, kuondoa umasikini, kuongeza ajira na Sekta hii imeziletea Maendeleo makubwa nchi zilizoendelea, kwa hiyo mkutano huu ni dhahiri kuwa sasa nchi za SADC zimeanza kuchukua hatua madhubuti za kukuza sekta hii na ikiwa mkakati huu utatekelezwa utasaidia kukuza uchumi wa nchi zetu”, Rais Magufuli.

Akielezea suala la teknolojia Rais Magufuli amesema kuwa ukuzaji wa teknolojia na ubunifu kwenye sekta ya viwanda ni silaha muhimu kwa nchi za SADC kuendelea na kutegemeana kwani utazalisha ajira, biashara kubwa, na kuepuka kuuza malighafi kwa wingi nje ya Afrika kama ilivyosasa.

Vilevile, mchango wa sekta ya viwanda kwa nchi za SADC bado ni mdogo kwani Sekta hiyo inachangia wastani wa asilimia 10 ya pato la taifa na katika Jumuiya ya SADC sekta hiyo muhimu inachangia asilimia 11 tu. Amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alizitaka nchi wanachama wa SADC kujikita zaidi katika kukuza ubunifu na teknolojia rahisi kwenye sekta ya viwanda kwa kuwaendeleza vijana na kuimarisha viwanda vidogo vidogo vilivyoko kwenye jumuiya, kwa hiyo wiki ya viwanda ni fursa muhimu kwa nchi zote wananchama.

“Wiki ya Viwanda ya SADC ni fursa ya kubadilishana uzoefu miongoni mwa wadau kuhusu utekelezaji wa mikakati ya miaka 49 ya uendelezaji wa viwanda katika jumuiya yetu, bado tunasafari ndefu kuhakikisha sekta ya viwanda inazidi kukua na kuleta mageuzi ya kiuchumi katika nchi zetu," Amesema Rais Magufuli

Rais Magufuli amesisistiza kwa kusema kuwa katika kuimarisha mashirikiano ndani ya Jumuiya ya Maendeleo (SADC) ni lazima kuimarisha sekta ya uwekezaji kwani nchi hizo zina fursa nyingi kwenye uwekezaji ikiwemo viwanda vya madini, kilimo, uvuvi na ufugaji kwa hiyo wananchi kutoka SADC wanatakiwa kuchangamkia fursa kwenye soko la takribani watu milioni 344.

Post a Comment

0 Comments