Windows

Galatasaray watua London kumtafuta Victor Wanyama




Maskauti wa kikosi cha Galatasaray cha Uturuki wametua jijini London, Uingereza kuanzisha mazungumzo yatakayomshuhudia kiungo Victor Wanyama akiondoka kwenye timu Tottenham Hotspur.

Kwa mujibu wa gazeti la Fanatik nchini Uturuki, ujumbe wa Galatasaray nchini Uingereza upo chini ya mkurugenzi wao wa soka Sukru Haznedar ambaye anatazamiwa kuwashawishi Tottenham kumwachilia nahodha huyu wa Harambee Stars kufikia Agosti 31, 2019.

Mbali na Wanyama, Galatasaray wanapania pia kujinasia huduma za kiungo matata wa Chelsea, Tiemoue Bakayoko kabla ya muhula wa usajili miongoni mwa vikosi vya Ligi Kuu ya Uturuki kumalizika rasmi mwishoni mwa mwezi huu.

Post a Comment

0 Comments