Windows

Zahera Kuwashuhudia ‘live’ Sibomana na Balinya

Mwinyi Zahera

KOCHA Mkuu wa Yanga, raia wa Dr Congo Mwinyi Zahera, leo Jumamosi atakuwa sehemu ya benchi la ufundi la Yanga akiwashuhudia kwa mara ya kwanza nyota wake wapya ambao wameshaanza kuonyesha makali yao, raia wa rwanda, Patrick Sibomana na Juma Balinya raia wa Uganda.

 

Hiyo ni katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir ya Burundi utakaochezwa leo Jumamosi kwenye Uwanja Chuo cha Biblia Bigwa mjini Morogoro.

Zahera hajawa sehemu ya benchi la ufundi la Yanga tangu timu hiyo ilipoingia kambini Julai 7, mwaka huu, kutokana na kuchelewa katika majukumu ya timu yake ya Taifa ya DR Congo na baadaye akaomba ruhusa kwenda kuiona familia yake nchini Ufaransa. Kwa mujibu wa Mratibu wa Yanga, Hafidhi Saleh, alfajiri ya leo Jumamosi, Zahera anawasili nchini kisha moja kwa moja kuingia kambini Morogoro kuungana na kikosi hicho ambacho baadaye saa 9 jioni kitakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir ya Burundi.


“Kocha wetu Mwinyi Zahera ilikuwa awasili leo (jana Ijumaa) lakini alikwama baada ya kutokea matatizo kidogo akiwa uwanja wa ndege huko Ufaransa, ila kwa taarifa yake amesema atashuka kesho (leo) Jumamosi alfajiri na atapitiliza moja kwa moja hadi hapa Morogoro ili tuwe naye kwenye mchezo wetu dhidi ya hao Warundi,” alisema Saleh.

EXCLUSIVE: ASKARI MSTAAFU ALIVYOZUIA WIZI WA MAGARI 10 | PART 2

The post Zahera Kuwashuhudia ‘live’ Sibomana na Balinya appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments