Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amekagua maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa shule ya msingi ya Mwisenge na kuridhishwa na kasi ya ukarabati huo.
Akizungumza baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ukarabati huo katika Shule aliyosoma Hayati Baba wa Taifa, Mwl.Julius Nyerere, Waziri Ndalichako alisema ameridhishwa na kasi hiyo ya ujenzi huo ambao unahusisha ukarabati wa majengo ya kale, ukarabati wa madarasa, mabweni, ujenzi wa madarasa mapya, uzio wa shule, mnara pamoja na uboreshashi wa mazingira. Mradi ambao unataraji kugharimu kiasi cha sh Milioni 706 ambazo zimetolewa na Wizara.
“Nimefurahishwa na hatua iliyofikiwa mpaka sasa na viwango vya ujenzi wa madarasa na mabweni nao ni imara, kwani hata ujenzi wa ukuta unafanyika vizuri, kuta za mabweni ni mrefu na utawafanya watoto wakilala ndani wapate hewa vizuri” alisema Prof. Ndalichako.
“Ni vizuri ndugu zetu wa Mambo ya Kale wafike mara moja ili kutoa muongoza wa namna bora wa kufanya ukarabati wa majengo haya ya kihistoria yanapaswa kukarabatiwa kuwezesha walioyosimamisha ili ujenzi huo uweze kukamilika mapema kuwezesha wanafunzi kupata fursa ya kuyatumia, kwani kuendelea kukwamisha ama kuchelewesha ukarabati huo ni kuchelewesha maelekezo ya Mhe. Rais," amesema.
Prof. Ndalichako amesema lengo la wizara ni kuona shule hiyo inakamilika mapema ili kutimiza maagizo aliyoyatoa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jonh Pombe Magufuli ya kutaka shule hiyo ikarabatiwe iwe na hadhi ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere aliyesoma shuleni hapo. Na kutoa maelekezo ya shule hiyo kuwa na hadhi ya Baba wa Taifa na kutatua kero ya watu kuvamia shule hiyo kwa kujengwa ukuta.
0 Comments