Watu wawili wamefariki dunia mkoani Pwani, kutokana na matukio tofauti ya mauaji yaliyotokea wilaya ya kipolisi Chalinze, ikiwa ni pamoja na Damian Kimiti (70) ambae ameuawa kwa kupigwa shoka.

Kufuatia mauaji hayo watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapo.

Akielezea kuhusiana na matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani hapo, kamanda wa polisi wa mkoa wa Pwani ,Wankyo Nyigesa alisema Kimiti aliuawa huko Malivundo,Talawanda ,Chalinze ambapo mtiliwa shaka Said Ngosha amekubali kuuwa na tayari amekamatwa.

Alisema baada ya mauaji muaji alipora simu tatu aina ya Tecno, solar panel moja, shuka na baiskeli.
“Pia alikubali kuonyesha simu tecno mbili ,solar panel moja na shoka moja,”alifafanua Wankyo.