Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Safaricom imemteua Michael Joseph kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa mpito baada ya Bob Collymore kufariki dunia Jumatatu 01/Julai/2019 baada ya kupigana vita vya miaka miwili na ugonjwa wa kansa.

Collymore atakumbukwa kwa utendaji uliotukuka, ulioigeuza Safaricom kuwa moja kati ya kampuni zinazoingiza faida kubwa Afrika Mashariki. Kwa sasa, kampuni ya Safaricom inathamani ya dola bilioni 11.