Takriban watu 13 wamefariki na wengine 4 kujeruhiwa kwa kiasi kikubwa baada ya baada ya ukuta wa mpaka kuporomoka mjini Mumbai nchini India asubuhi hivi leo baada ya mvua kubwa kugonga mji huo kwa siku chache zilizopita.
Kuna uwezekano watu zaidi ya watano wamekwama chini ya vifusi hivyo,msemaji kutoka kiini cha usimamizi wa maafa ya Manispaa ya Mumbai alisema kuwa timu ya Jeshi la Maafa ya Taifa pamoja na wazima moto na polisi wanaendelea katika operesheni za uokoaji.
Hili ni tukio la pili la kuporomoka kwa ukuta, siku ya Jumamosi watu wasiopungua 15 walifariki baada ya ukuta kuporomoka makazi duni huko Kondhwa mjini Pune, kilomita 162 kusini mashariki mwa Mumbai.
Mji wa Mumbai umeshuhudia mvua kali katika siku chache zilizopita,mvua ambayo imekuwa ikisababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi.
0 Comments