BEKI wa kimataifa wa Simba, Pascal Wawa, amefunguka kuwa hana hofu na nafasi yake ndani ya kikosi hicho, kazi ni kwake kupambana kisha kocha Aussems ndiyo ataamua ampange nani.
Mabeki wa kati watakaowania namba na Wawa Simba ni Gerson Fraga, Kennedy Juma, Erasto Nyoni na Yusuph Mlipili. Wawa ni mmoja kati ya wachezaji ambao waliipambania Simba msimu uliopita kuiwezesha kutwaa ubingwa wa ligi kuu na kuifikisha robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Akizungumza na Championi Ijumaa akiwa Afrika Kusini ‘Sauz’ ambako Simba imepiga kambi ya maandalizi, Wawa alisema kuna mabadiliko ndani ya kikosi chao na kuna ongezeko la baadhi ya nyota katika nafasi anayocheza, ila hilo halimsumbui, zaidi ni kupambana.
“Kikosi chetu kina mabadiliko kwenye safu ya ulinzi, lakini hilo haliwezi kunipa hofu mimi kwamba siwezi kupata nafasi, sababu najua mwalimu ataamua nani acheze kutokana na kuangalia kiwango bora kati yetu, ndiyo maana sina hofu.
“Kama sasa maandalizi yanakwenda safi kabisa, hali ya hewa nzuri, hivyo kila kitu sawa na kocha amekuwa akifanyia kazi sana eneo la ulinzi kwa bidii kuweka mambo sawa, ili kuwa na safu bora ya ulinzi,” alisema Wawa.
EXCLUSIVE 3: KAJALA Azungumzia MAFANIKIO yake..
The post Wawa awavimbia mabeki Simba appeared first on Global Publishers.
0 Comments