Windows

Afghanistan: Watu nane wafariki na wengine 27 kujeruhiwa baada ya milipuko mitatu


Watu wasiopungua nane wamefariki na wengine 27 kujeruhiwa baada ya milipuko mitatu kutokea katika mji mkuu wa Kabul nchini Afghanistan hivi leo (Alhamisi) asubuhi. Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Nasrat Rahimi alisema.

Kulingana na Rahimi, mlipuko wa kwanza ulilenga basi ndogo la wizara ya migodi iliyobeba wafanyikazi wake katika Wilaya ya Polisi ya 16 saa 8:10 asubuhi na kusababisha vifo vya watu watano na kujeruhi wengine 12 wakiwemo wanawake na watoto.

Mlipuko wa pili ulitokea karibu eneo hilo hilo dakika chache tu baada ya mlipuko wa kwanza lakini hakuna majeruhi wowote waliripotiwa.

Mlipuko wa tatu ulitokea katika wilaya ya polisi ya 9 na kusababisha vifo vya raia watatu na kujeruhi wengine 15. Hakuna kundi lolote limedai kuhusika na mashambulizi hayo lakini maafisa wa usalama wanalaumu kundi la kigaidi la Taliban.

Post a Comment

0 Comments