Windows

Serikali ya China na Tanzania kuzidi kushirikiana katika kupambana na Malaria

SERIKALI YA CHINA NA TANZANIA KUENDELEZA USHIRIKIANO KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA

Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imeahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya Malaria ili kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi salama isiyo ya maambukizi ya Ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya kutoka Uchina Mhe. Lin Bin alipotembelea Ikwiriri, Rufiji Mkoa wa Pwani katika mradi wa ushirikiano wa pamoja baina ya China na Tanzania katika kudhibiti ugonjwa wa malaria huku akiongozana na mwenyeji wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu.

“China kuwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kimatafa tutaendelea kushirikiana kwa pamoja katika kusaidia Tanzania inafikia malengo ya kutokomeza ugonjwa wa malaria” amesema Mhe. Lin Bin na kuendelea kusema Ugonjwa wa malaria unatibika na kuzuilika.

Waziri Lin Bin amesema kuwa ushirikiano baina ya Tanzania na China umeleta manufaa katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria kwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo Wilayani Rufiji kutoka asilimia 25 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 4.9 mwaka 2019.

Kwa upande wake Waziri wa Afya Tanzania, Mhe. Ummy Mwalimu ameishuruku Serikali ya China inayoongozwa na Rais Xi Jinping kwa kuendeleza ushirikiano wa enzi uliopo wa baina ya nchi hizo.

“Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli tumechukua hatua mbali mbali kwa kushirikiana na wadau wakiwemo China kupambana na malaria na yapo mafanikio makubwa ambayo tumeyapata” Amesema Waziri Ummy Mwalimu na kuendelea “Tumeweza kupunguza kiwango cha maambukizi ya malaria kutoka asilimia 14.7 mwaka 2015 hadi 7.3 mwaka 2018”

Amesema kuwa wagonjwa wapya wa malaria wamepungua kwa asilimia 26 kutoka watu 161 katika kila watu 1000 mwaka 2014 hadi kufikia 119 katika kila watu 1000 mwaka 2018 huku vifo vitokanavyo na malaria vimepungua kwa asilimia 55, kutoka vifo 20 katika watu 1000 mwaka 2014 hadi kufikia vifo 9 kati ya watu 1000 mwaka 2018.

“Serikali ya Tanzania itaendela kuchukua hatua kwa kushirikiana na wadau wetu wakiwemo Serikali ya China kuhakikisha tunapunguza kiwango cha maambukizi"



Post a Comment

0 Comments