Windows

Wachezaji wa Simba SC waliojiunga na kambi ya Taifa Stars


Wachezaji Simba SC, John Bocco, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Aishi Manula, Hassan Dilunga, Jonas Mkude na Ibrahim Ajibu wamerejea nchini kujiunga na kambi ya Taifa Stars.

Kikosi cha Taifa Stars kipo kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za CHAN ambao watacheza na timu ya Taifa ya Kenya.

Ikumbukwe kwa sasa kikosi cha Simba SC kipo mjini Rusternburg nchini Afrika Kusini ambako kimeweka kambi kujiandaa na msimu mpya  wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL) na Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).



Post a Comment

0 Comments