Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mageni rasmi katika ufunguzi wa maonensho ya wiki ya Viwanda kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yatakayofanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 5, 2019.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini humo Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amewaasa Watanzania kujitokeza kwa wingi na kutumia fursa ya maonesho ya wiki hiyo yatakaofanyika kwa lengo la kuhamasisha na kukuza ujenzi wa uchumi wa viwanda na kukuza masoko kwa nchi wanachama.
“Tayari washiriki 580 wameshajiandikisha kushiriki maonesho hayo na matarajio yakiwa washirki zaidi ya 1000 kutoka katika nchi wanachama wa SADC na tunachoangalia kwa sasa ni namna maonesho ya wiki ya viwanda yatakavyowanufaisha Watanzania kwani hii ni fursa ya wazalishaji wetu na wamiliki wa viwanda kutangaza bidhaa zao na kupanua wigo wa masoko katika nchi wanachama,“ Alisisitiza Bashungwa.
0 Comments