Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amefanya ukaguzi wa pamba iliyohifadhiwa katika vijiji vya Mbutu na Mwabhakima wilayani Igunga wakati akihitimisha ziara ya siku mbili mkoani Tabora iliyokuwa na lengo la kufuatilia kwa karibu na kujiridhisha hali hali halisi juu ya masoko kwa ujumla.
Waziri mkuu Majaliwa amewahakikishia wakulima kuanzia sasa zao hilo litaanza kununuliwa kwa pesa taslimu badala ya mkopo baada ya kutengeneza utaratibu wa kusaidia wanunuzi kuweza kupata pesa kwenye taasisi za kifedha ili waweze kumudu kununua pamba kwa wingi.
Wilaya ya Igunga ndiyo kinara wa uzalishaji wa pamba kwa Mkoa wa Tabora ambapo inazalisha wastani wa asilimia 94 ya pamba yote inayolimwa mkoani Tabora ambapo kwa msimu huu imezalisha pamba kilo milioni 42.
0 Comments