Windows

Shirika la anga India lasitisha ya kuelekea mwezini


Shirika la anga la India limesitisha safari ya pili ya kuelekea mwezini hapo jana kutokana na hitilafu za kiufundi katika chombo chake cha Chandrayaan-2, kilichotakiwa kufanya safari hiyo.

Hata hivyo, Shirika hilo limesema tarehe mpya ya kuanza kwa safari hiyo itatangazwa baadaye.

Safari ya chombo hicho kuelekea mwezini ilipangwa kuanza usiku wa kuamkia jana na ilitarajiwa kutua katika upande ulio mbali kidogo na mwezi kwa lengo la kuchunguza uwepo wa maji katika eneo hilo.

Ujumbe wa kwanza wa Chandrayaan-1 wa mwaka 2008 uliofika mwezini uliwahi kuthibitisha kuwepo kwa maji kwenye mwezi.

Post a Comment

0 Comments