Na. Amiri kilagalila, Njombe
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa amemuagiza mkandarasi wa ujenzi wa barabara kiwango cha lami Njombe-Morongo kuelekea wilayani Makete kukamilisha km 36 kati ya 53.9 za ujenzi huo ifikapo novemba mwaka huu.
Kwandikwa ametoa maagizo hayo kwa mkadarasi China Henan International Cooperational Group wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa bara bara hiyo mala baada ya kubadilishwa kwa baadhi ya wataalamu waliokuwa wakififisha maendeleo ya mradi huo.
“Ninachotaka mkandarasi sasa aongeze kasi ili kazi isisimame mpaka novemba angalau tuwe tumekamilisha mwezi novemba kwa kiwango cha lami,na namna walivyojiandaa tumeona material kule yapo na lami ipo kwa hiyo maelekezo yangu waongeze kasi ili twende na mda ule uliopangwa”alisema kwandikwa
Aidha amewahakikishia wananchi wa Njombe na wilaya ya Wanging’ombe zilipo km hizo kupata huduma ya barabara hiyo mapema ili iweze kuchangia katika uchumi.
Lusekelo kijalo ni injinia wa mradi huo amekiri kukamilisha mapema mradi huo kutokana na maelekezo ya waziri kwa kuwa mpaka sasa kazi kazi iliyobakia ni ndogo ukilinganisha na awali.
“Kabla ya Novemba tutakuwa tumemaliza km 36 na bado tunaendelea na kazi za kunyanyua tuta ambapo mpaka sasa tumebakiza km 6 ambazo kabla ya mvua tutakuwa tumemaliza tutabaki lea ya juu kama CI na CRR na kama tutaweza kufanya CI kabla ya mvua CRR tutaweza kumaliza pia kipindi cha mvua kwasababu yenyewe inahitaji maji mengi”alisema Eng.Lusekelo kijalo
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Ally kasinge amewaelekeza wananchi kuhakikisha maeneo ya mradi huo yanakuwa salama,huku akiwashukuru baadhi ya wananchi wanaoendelea kujitoa kuhakikisha usalama wa vifaa vya ujenzi pamoja na kusaidia kutoa taarifa kwa jeshi la polisi juu ya wanaohujumu mradi huo.
Mradi wa ujenzi wa kipande cha barabara Njombe-Morongo kuelekea Makete unaogalimu shilingi 107,085,360,088 ni miongoni mwa vipande vya barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami kuelekea wilayani Makete mkoani Njombe unategemewa kukamilika januari 2 2020 kutokana na miezi 29 aliyopewa mkandarasi huyo.
0 Comments