Windows

Watakiwa kuwaendeleza kielimu watoto wanaoishi mitaani


Wananchi mkoani Njombe wametakiwa kuwaendeleza kielimu watoto wanaoishi mitaani.

Hayo yamesemwa na afisa ustawi jamii Wa halmashauri ya mji wa makambako Rejis Ng’itu wakati akizungumza na mtandao huu ofisini kwake  baada ya kukutana na watoto wawili mmoja akiwa na umri wa miaka 15 na mwingine miaka 7 wakazi wa mtaa wa jeshini mjini makambako ambao wameacha shule na kuingia kwenye ajira isiyo rasmi ya kutengeneza kamba,vikapu na mikeka kwa kutumia plastiki kutokana na kukosa mahitaji muhimu kutoka kwa wazazi wao.

"Mtoto wa mtaani siyo mtoto ambaye ameshindikana hawezi kubadilishika hapana,hakuna kiumbe chochote kisichobadilishika hasa binadamu kwa hiyo ni changamoto tu ambazo anakumbana nazo inawezekana ni changamoto ambazo zinamsukuma kutoka nyuma yake au nyingine ambazo zinamvuta mbele yake kwa hiyo ni vitu vya kawaida wanaweza kubadilika tusiwachukulie tofauti lakini lengo kubwa ni kuweza kuwasaidia"amesema Ng’itu

Aidha Ng’itu ameongeza kuwa kutokana na hali za watoto hao ambao mmoja aliishia darasa la sita na mwingine  chekecheka,atazungumza na viongozi wa halmashauri ili kuona namna na kuwarudisha shule wakapate elimu  ambayo itawasaidia kutimiza ndoto zao.

"Hizi taratibu lazima tuzianze mwaka huu ili kuweza kuangalia kwa sababu kama mmoja ameanza chekechea kwa hiyo tutafanya utaratibu kwamba mwaka huu kabla haujaisha tuwe na uhakika kwamba mtoto huyu ataanza shule mwakani,na huyu mwingine   kama kunauwezekano kama memkwa wataweza kumpokea karibuni basi aweze kwenda shuleni mwaka huu na mwakani ataendelea kama atakubaliwa kurudi katika utaratibu wa kawaida kwa taratibu ambazo zipo katika kitengo husika basi aweze kurudi"amesema Ng`itu

Nao walezi wa watoto hao wamesema kuwa hawakupenda kuona watoto hao wana acha shule bali ni kutokana na changamoto za wazazi wao  kutengana kwenye ndoa na kuwaacha bila masaada wowote.

"Huyu mtoto ana baba na mama lakini walitengana hawa wazazi wawili mimi kama babu yao niliamua kuwachukua na kukaa nao yani kama kijinsia inatakiwa kama mmeamua kuzaa watoto mnatakiwa kushirikiana kuwatunza watoto, na mimi sipendi aende mtaani isipokuwa alimchukua shangazi yake kwa madai kwamba ananyanyasika nyumbani kwangu"

Kwa upande wa watoto hao wamesema waliacha shule kutokana na wazazi wao kutengana na kushindwa kupata mahitaji yao hivyo wameiomba jamii iwasaidie ili waweze kurudi shule.

"Nilianza chekechea kila nikisoma namaliza baba hataki kunipepeka la kwanza ndo baba akasema niende kukaa kwa bibi na babu alitaka niende shuleni lakini bibi akasema wazazi wenu wamekaa huko wanakula maisha mazuri sisi ndo tuanze kuwasomesha mtajua na wazazi wenu na mama alishanikimbia,na mimi lilikuwa nakaa na bibi mama angu alinikimbia naomba tu nisaidiwe nirudi shuleni"

Migogoro ya wazazi katika familia inatajwa ni moja ya sababu kubwa ambayo inayoathiri elimu na malezi bora ya watoto.

Post a Comment

0 Comments