Windows

Kwa Shikalo! Kindoki atulie Tu

KIPA mpya wa Yanga raia wa Kenya, Farouk Shikalo, amejikuta akiwapagawisha mashabiki wa timu hiyo ambao wamekuwa wakijazana katika Uwanja wa Highlands Park nje kidogo ya Mji wa Morogoro kushuhudia mazoezi ya timu hiyo.

 

Kwenye mazoezi ya jana Ijumaa, Shikalo alizikonga nyoyo za mashabiki hao baada ya kuonyesha umaridadi mkubwa wa kunyaka kila mpira aliopigiwa langoni na kocha wake, Peter Manyika hukua wakidai ndiye mbabe wa Klaus Kindoki ambaye naye alikuwepo mazoezini hapo.

Shikalo amejiunga na Yanga hivi karibuni akitokea katika Klabu ya Bandari ya Kenya ingawa alichelewa kuingia kambini kufuatia klabu yake hiyo ya zamani kuwa katika michuano ya Kagame Cup nchini Rwanda.

 

 

Championi ni gazeti pekee lililoweka kambi yake mkoani Morogoro kuhakikisha linakuletea habari zote za kambi ya Yanga, ambapo kwenye mazoezi hayo Shikalo aliwafurahisha vilivyo mashabiki wake baada ya kunyaka kila mpira aliopigiwa na Manyika lakini hata walipoanza kucheza kama timu alionekana kutokubali kufungwa kizembe.

Kuna muda mashabiki waliokuwa uwanjani hapo walisikika wakitambiana kuwa kwa sasa wamepata suluhisho lao kwani ukimtafuta David De Gea wa Manchester United, basi kwa msimu huu anapatikana Yanga pekee. Kwa upande wake, Shikalo alizungumza kifupi kwa kusema: Nimekuja kufanya kazi.”

The post Kwa Shikalo! Kindoki atulie Tu appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments