Windows

Joseph Kimwaga kutoka Azam FC atua Biashara United


Mchezaji wa zamani wa timu ya Azam FC Joseph Kimwaga amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia klabu ya Biashara United Mara inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mara baada ya kusaini mkataba wake Kimwaga amesema amefurahi kujiunga na timu hiyo kwani atapata nafasi nzuri ya kuonesha kiwango chake.

Katika hatua nyingine, klabu hiyo pia imekamilisha usajili wa Mushta Khamis kutoka African Lyon kwa mkataba wa mwaka mmoja.



Post a Comment

0 Comments